Vipengele vya mfumo
SkyStock ni mfumo wa usimamizi wa biashara ambao unakuwezesha kufuatilia mwenendo wa mauzo katika biashara, kuwa na uhakika wa uwepo wa bidhaa katika stock na uwezo wa kufahamu ukuaji wa biashara kwa kujua faida halisi zinazopatikana.
Anza kutumia/Register
Sajili bidhaa
mfumo unakuwezesha kufanya usajili wa bidhaa zote zilizopo dukani, usajili hufanyika moja kwa moja kwenye mfumo au kwa kupakia bidhaa zilizopo kwenye excel.
Simamia stock
Mfumo unakuwezesha kuweka taarifa za idadi ya kila bidhaa iliyopo dukani au inayonunuliwa. Taarifa hizi zitasaidia kufahamu bidhaa zinazobaki kwenye stock kila baada ya mauzo kufanyika pamoja na kufahamu faida ya biashara endapo bidhaa hizo zitauzwa
Fanya Mauzo
Taarifa zote za mauzo zitahifadhiwa kwa kuzingatia bidhaa ambazo zimeuzwa kwa wateja, kwa kila mauzo yanayofanyika bidhaa katika stock zitakuwa zinapungua
Simamia wafanyakazi
Usajili wa wafanyakazi katika biashara utafanyika kwa kuzingatia majukumu aliyonayo ili kuepuka wizi na udanganyifu. Mmiliki wa biashara ataweza kuongeza au kuondoa wafanyakazi muda wowote
Tunza taarifa za matumizi katika biashara
Matumizi yote yanayofanyika ndani ya biashara yatahifadhiwa kwenye mfumo ili kufahamu faida halisi ya biashara baada ya kutoa matumizi yote yaliyofanyika
Mauzo kwa mkopo
Mfumo unaruhusu kufanya mauzo kwa mkopo na mteja atakuwa akifanya malipo kidogo kidogo katika deni lake la bidhaa alizokopa. Hii inarahisisha kufahamu wateja ambao wanadaiwa
Tunza taarifa za malipo kabla
mfumo unaruhusu kuhifadhi taarifa za wateja wanaojiwekea akiba kwa ajili ya kuja kuchukua bidhaa fulani, mteja anapofikia lengo lake kulingana na gharama ya bidhaa anazohitaji mauzo yatafanyika kwa kutumia hiyo fedha aliyowekeza
Pata ripoti mbalimbali katika mfumo
Ripoti za mauzo, bidhaa zilizopo stock, matumizi n.k, zote zinapatikana muda wowote, hii itarahisisha kufahamu mwenendo wa biashara yako kila siku pasipo kufika duka
Gharama
Gharama zetu ni nafuu sana, hakuna sababu ya kutokutumia kwani zinalipika
Tarangire
2,500 / Mwezi
- Akaunti 1
- Bidhaa: Bila kikomo
- Invoice: Bila kikomo
- Staff: Bila kikomo
Ngorongoro
5,000 / Mwezi
- Akaunti 3
- Bidhaa: Bila kikomo
- Invoice: Bila kikomo
- Staff: Bila kikomo
Serengeti
7,500 / Mwezi
- Akaunti: Bila kikomo
- Bidhaa: Bila kikomo
- Invoice: Bila kikomo
- Staff: Bila kikomo
Wasiliana nasi
Ofisi zetu zipo Dodoma, Kwa kutumia mtandao tunahudumia wateja wetu Tanzania nzima