Vipengele vya mfumo

 SkyStock ni mfumo wa usimamizi wa biashara ambao unakuwezesha kufuatilia mwenendo wa mauzo katika biashara, kuwa na uhakika wa uwepo wa bidhaa katika stock na uwezo wa kufahamu ukuaji wa biashara kwa kujua faida halisi zinazopatikana.
  Anza kutumia/Register

 Sajili bidhaa

 mfumo unakuwezesha kufanya usajili wa bidhaa zote zilizopo dukani, usajili hufanyika moja kwa moja kwenye mfumo au kwa kupakia bidhaa zilizopo kwenye excel.   

 Simamia stock

 Mfumo unakuwezesha kuweka taarifa za idadi ya kila bidhaa iliyopo dukani au inayonunuliwa. Taarifa hizi zitasaidia kufahamu bidhaa zinazobaki kwenye stock kila baada ya mauzo kufanyika pamoja na kufahamu faida ya biashara endapo bidhaa hizo zitauzwa

 Fanya Mauzo

 Taarifa zote za mauzo zitahifadhiwa kwa kuzingatia bidhaa ambazo zimeuzwa kwa wateja, kwa kila mauzo yanayofanyika bidhaa katika stock zitakuwa zinapungua

 Simamia wafanyakazi

 Usajili wa wafanyakazi katika biashara utafanyika kwa kuzingatia majukumu aliyonayo ili kuepuka wizi na udanganyifu. Mmiliki wa biashara ataweza kuongeza au kuondoa wafanyakazi muda wowote

 Tunza taarifa za matumizi katika biashara

 Matumizi yote yanayofanyika ndani ya biashara yatahifadhiwa kwenye mfumo ili kufahamu faida halisi ya biashara baada ya kutoa matumizi yote yaliyofanyika

 Mauzo kwa mkopo

 Mfumo unaruhusu kufanya mauzo kwa mkopo na mteja atakuwa akifanya malipo kidogo kidogo katika deni lake la bidhaa alizokopa. Hii inarahisisha kufahamu wateja ambao wanadaiwa

 Tunza taarifa za malipo kabla

 mfumo unaruhusu kuhifadhi taarifa za wateja wanaojiwekea akiba kwa ajili ya kuja kuchukua bidhaa fulani, mteja anapofikia lengo lake kulingana na gharama ya bidhaa anazohitaji mauzo yatafanyika kwa kutumia hiyo fedha aliyowekeza

 Pata ripoti mbalimbali katika mfumo

Ripoti za mauzo, bidhaa zilizopo stock, matumizi n.k, zote zinapatikana muda wowote, hii itarahisisha kufahamu mwenendo wa biashara yako kila siku pasipo kufika duka

Ni rahisi kutumia

Huhitaji kuwa na uzoefu waziada kuweza kutumia mfumo huu, kwani umetengenezwa kumuwezesha mtu yeyote kutumia

Gharama

Gharama zetu ni nafuu sana, hakuna sababu ya kutokutumia kwani zinalipika 

Tarangire

2,500 / Mwezi

 • Akaunti 1 
 • Bidhaa: Bila kikomo
 • Invoice: Bila kikomo
 • Staff: Bila kikomo

Ngorongoro

5,000 / Mwezi

 • Akaunti 3 
 • Bidhaa: Bila kikomo
 • Invoice: Bila kikomo
 • Staff: Bila kikomo

Serengeti

7,500 / Mwezi

 • Akaunti: Bila kikomo 
 • Bidhaa: Bila kikomo
 • Invoice: Bila kikomo
 • Staff: Bila kikomo

Wasiliana nasi

Ofisi zetu zipo Dodoma, Kwa kutumia mtandao tunahudumia wateja wetu Tanzania nzima

Tuachie ujumbe